Skip to main content
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, Wilaya ya Tarime kaskazinimagharibi mwa Tanzania © 2022 Private

(Nairobi) – Polisi nchini Tanzania  wanaolinda Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wamehusishwa na mauaji ya angalau watu sita na kujeruhi wengine kadhaa wakati wa migogoro na wananchi kuanzia mwezi Februari 2024, Huma Rights Watch imesema hii leo. Mamlaka nchini Tanzania hazina budi kufanya uchunguzi huru na usio na upendeleo juu ya mauaji na unyanyasaji mwingine katika wilaya ya Tarime iliyoko Kaskazini mwa Tanzania.

Polisi wamewatuhumu wale waliouliwa na kujeruhiwa kwa makosa ya “kuvamia migodi” na kuendesha uchimbaji mdogo kinyume cha sheria ndani ya eneo la mgodi. Polisi hawajakamata mtu yeyote kutokana na makosa hayo.

"Kuongezeka kwa idadi ya mauaji yasiyochukuliwa hatua yanayohusishwa na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara nchini Tanzania kunaakisi hali inayotia wasiwasi ya kutoadhibiwa kwa unyanyasaji ijambo ambalo linahitaji kushughulikiwa" asema Oryem Nyeko, Mtafiti Mkuu wa Human Rights Watch Tanzania, “Mamlaka nchini Tanzania hazina budi kushughulikia kesi hizi na kuhakikisha wale wanaohusika wanawajibishwa na kuepuka kuzificha au kuzipuuza.”

Mwaka 2014, Serikali ya Tanzania iliingia makubaliano na t kampuni ya Mgodi wa Dhahabu ya North Mara ya kulinda mgodi huo kwa kuwa na hadi maafisa wa polisi 110, wanaojulikana na wanajamii kama “polisi wa mgodi”. Vikundi vya haki za binadamu na wanajamii wameripoti kwamba kufuatia makubaliano haya maafisa wa polisi wamehusishwa na kuwapiga, kuwafyatulia risasi, kuwatesa na kuwaweka kuzuizini bila kuwashitaki wakazi wa maeneo karibu na mgodi. Polisi wanawatuhumu wakazi s kwa uwizi katika mgodi na maeneo yanayozunguka sehemu ya kutupa taka zitokanazo na uchimbaji katika mgodi. 

Barrick Gold, kampuni ya madini yenye makao makuu yake Toronto, Canada na serikali ya Tanzania kwa pamoja wanamiliki mgodi wa Dhahabu wa North Mara tangu mwaka 2019. Eneo hili ni makazi ya Wakurya ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uchimbaji mdogo katika ardhi hiyo kwa karne kadhaa. Mwaka 2022, Watanzania 21 waliwashitaki Barrick Gold  kwenye mahakama nchini Canada, wakiituhumu kampuni hiyo kushiriki katika mauaji ya kiholela na kupigwa kwa wakazi kunakofanywa na polisi wanaolinda mgodi. Wanadai kuwa kampuni imebadilisha wanaofanya kazi ya ulinzi mgodini “kuwa kikosi binafsi kinachobeba silaha nzito.” Kesi hii imepangwa kusikilizwa kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba.

Katika miezi minne iliyopita vifo na majeruhi kadhaa vimeripotiwa ambapo hakuna mtu aliyekamatwa. Polisi waliripotid kuwa mnamo Februari 28, Jackson Nyamonge, miaka 28 mkazi wa Kijiji cha Nyamwaga alikutwa amefariki katika uzio wa mgodi akiwa na majeraha kifuani na tumboni. Mnamo Aprili 7, vyombo vya Habari viliripoti kuwa polisi walimfyetulia risasi Sylvester Sobhe Marwa Nyangige iliyompata kichwani wakati wa operesheni ya ulinzi mgodini. Nakala ya fomu ya polisim, iliyoonekana na Human Rights Watch inaeleza “kifo kisicho cha kawaida” kama mazingira ya kifo chake. Mwezi Aprili 26, polisi wanadaiwa kumfyetulia risasi na kumjeruhidmguuni Pascal Malembara katika eneo la Murwambe. 

Mnamo Mei 6, polisi walithibitisha kifo cha Emmanuel Nyakorenga, mkazi wa Kijiji cha Kewanja katika shule ya msingi karibu na Kijiji cha Nyabigena, eneo karibu na mgodi. Polisi walivieleza vyombo vya habaria kuwa alikuwa sehemu ya kikundi cha watu waliokuwa na “silaha za jadi” ambao waliwashambulia maafisa wa polisi ambao walikuwa wanawazuia kuingia eneo la mgodi kinyume cha sheria.  

Shuhuda mmoja alielezea mauaji ya Nyakorenga, aliwaeleza Human Rights Watch kuwa muda wa saa kumi na mbili jioni, polisi walionekana wakiwakimbiza watu kadhaa kutoka eneo la Gokona karibu na mgodi kuelekea viwanja vya michezo vya Shule ya Msingi Nyabigena, takribani mita 500 kutoka mgodini. Polisi wanadaiwa waliwafyatulia watu hao mabomu ya machozi, mabomu ya sauti na risasi za moto na kuwajeruhi baadhi yao.   

Muda mchache baada ya Nyakorenga kufyatuliwa risasi, maafisa wa polisi waliondoka na wakazi wa eneo hilo waliweka vizuizi barabarani karibu na shule kupinga mauaji ya Nyakorenga. Baadae polisi walirudi na kuwatawanya watu, kwa kutumia mabomu ya machozisNdugu wa Nyakorenga d walisema kuwa ripoti ya uchunguzi baada ya kifo ilikuta kitu kilichoonekana kama risasi kichwani kwake lakini maafisa waliofanya uchunguzi huo hawakuwapa taarifa zaidi. 

Tangu Mei 6, wakazi wameripoti vifo vya angalau watu wengine watatu katika eneo hilo. Siku moja baada ya kifo cha Nyakorenga, wakazi waliripoti kuwa walipata mwili wa mtu mwingine asiyefahamika ukiwa katika eneo la kutupa taka za mgodi nje ya eneo la mgodi. Mwezi Mei 22, vyombo vya habari viliripoti d kuwa Babu Christopher Iroga mkazi wa Kijiji cha Mjini Kati na July Mohali mkazi wa Kijiji cha Nyangoto waliuwawa wakati wa majibizano na polisi. Polisi waliwatuhumu watu hawa kwa wizi katika mgodi.

John Heche, mbunge wa zamani wa Wilaya ya Tarime aliiambia Human Rights Watch kuwa unyanyasaji wa polisi umekithiri katika miaka ya karibuni, akisema: “Kwa miaka kadhaa vifo hivi vimekuwa vikitokea lakini sio kwa kiwango hiki. Watu wanafyetuliwa risasi karibu kila siku.”

Barrick Gold ilisema katika majibu yake ya Juni 11 e ya maombi ya taarifa kutoka Human Rights Watch ya Juni 4 kuwa kampuni “haina na haiwezi kuwa na udhibiti wowote juu ya polisi na vitendo vyao,” na kwamba “polisi huombwa kuingia eneo la mgodi kutoa msaada wa kusimamia sheria na utulivu” pale maisha ya wafanyakazi yanapokuwa hatarini.  Kampuni ilisema kuwa “hawahusiki kwa hali yoyote au kufahamu kuhusu vitendo vya  [Jeshi la Polisi la Tanzania] katika jamii, na haiwezi kuwajibika kwa vitendo hivyo kwa kuwa tu vitendo hivyo vinafanyika eneo lililo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.”

Sera ya haki za binadamuy ya Barrick Gold inaeleza kuwa “hatutovumilia uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na wafanyakazi wetu, washirika wetu au wahusika wowote wanaofanya kazi kwa niaba yetu au wanaohusika na neo lolote katika shughuli zetu,” na kwamba inafanya “jitihada zote kuepuka kuhusika katika madhara ya uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na kufaidika na vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na wengine.”

Chini ya Kanuni za Miongozo za Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Haki za Binadamu, kampuni zinawajibu wa kuepuka kusababisha au kuchangia uvunjifu wa haki za binadamu na kutoa fidia kwa waathirika wa unyanyasaji waliosababisha au kuchangia.

Kanuni za Msingi za UN kuhusu Matumizi ya Nguvu na Silaha za Moto kwa Maafisa Wanaosimamia Utekelezaji wa Sheriaszinawataka polisi kutumia njia zisizokuwa za nguvu kabla ya kuamua kutumia nguvu na silaha za moto. Wajibu wa maafisa wanaosimamia sheria ni kulinda mali na maisha, na wanapaswa kutumia nguvu pale tu inapolazimu na kwa kiasi na kutumia nguvu za ziada pale tu inapokuwa ni lazima kufanya hivyo ili kuokoa maisha.

“Kwa miaka mingi wakazi wa maeneo ya karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara nchini Tanzania wamelalamika kuhusu ukatili unaofanywa na polisi,” alisema Nyeko. “Serikali ya Tanzania haina budi kuhakikisha upelelezi huru na usio na upendeleo kuhusu unyanyasaji huu ili waathirika na familia zao wapate haki.”

Correction

Shuhuda akielezea mauaji ya Nyakorenga, aliwaeleza Human Rights Watch kuwa majira ya saa 12 jioni maafisa wa polisi waliwakimbiza watu kadhaa kutoka eneo karibu na mashimo ya Gokona kuelekea viwanja vya michezo vya Shule ya Msingi wa Nyabigena takriban mita 500 kutoka eneo la mgodi. 

Your tax deductible gift can help stop human rights violations and save lives around the world.

Region / Country